Ofisi ya haki za binadamu yaitaka Israel ikome ubomoaji wa makazi ya Wapalestina

24 Septemba 2013

Serikali ya Israel imelaumiwa kutokana na kitendo chake cha uendeshaji bomoa bomoa kwa makazi ya Wapalestina yaliyoko katika eneo la Ukingo wa Gaza.

Inakadiriwa kwamba katika kipindi cha Septemba 16, zaidi ya majengo 58 yalikuwa yamebomolewa ikiwemo yale yaliyokusudiwa kwa ajili ya makazi ya raia.

Mamia ya familia ikiwemo watoto wadogo wanataabika kutokana na kukosa makazi . Ofisi ya haki za binadamu imeitaka Israel kusitisha mpango wake huo wa ubomoaji kwa vile unakiuka haki za msingi za mtu kupata makazi na kuisnhi.

Ofisi hiyo imesema kuwa kitendo hicho kinakwenda kinyume na mkataba wa Geneva kipengele na 49 kinachotoa haki kwa mtu kupata makazi bora na kuishi