Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto badio wanateseka kufuatia mgogoro Syria:UNICEF

Watoto badio wanateseka kufuatia mgogoro Syria:UNICEF

Wakati mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza kesho mjini New York shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaonya kwamba ni lazima watoto wanoteseka kufuatia vita vinavyoendelea nchini Syria wakombolewe.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Anthony Lake amesema kuendelea kwa vita nchini humo kunamaanisha kuendelea kutopata huduma kwa watoto kama vile chanjo, maji salama ya kunywa, malazi, elimu na msaada wakisaikolojia.

Amesema lazima watopto wafikiwe haraka na bila vikwazo na kuzitaka pande zinazopigana kuruhusu wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu kuwafikia ili kuitoa misaada ya kuokoa maisha .

Bwana Lake amesema njia mojawapo ya kuwakomboa watoto hao ni kutumia kampeni ya nne ya ya chanjo katika siku ya afya ya mtoto, inayokusudia kuwalinda watoto laki saba ambao hawajafikiwa na kampeni ya chanjo ya hivi karibuni.