Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je mtoto unaweza kuchora picha kuonyesha athari za utupaji chakula kwa mazingira duniani?

Je mtoto unaweza kuchora picha kuonyesha athari za utupaji chakula kwa mazingira duniani?

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP limeandaa shindano la kimataifa la uchoraji picha kuhusu kuokoa sayari ya dunia kwa kuepuka utupaji chakula. Shindanohilomahsusi kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka Sita hadi 14 litafikia kilele mwakani ambapo ukomo wa kuwasilisha picha zilizochorwa ni tarehe 15 mwezi Machi mwaka 2014. Katika kuhamasisha watoto barani Afrika kushiriki shindanohilo, UNEP kanda ya Afrika ina ujumbe huu!