Rais wa baraza kuu asisitiza suluhu ya kisiasa Syria

12 Septemba 2013

Mustakabali wa Syria ni muhimu katika usalama na ustawi wa ukanda mzima wa mashariki ya mbali na pengine dunia nzima kwa ujumla.

Hiyo ni kauli ya Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Vuk Jeremic katik ataarifa yajke alioitoa leo mjini New York wakati akizungumzia mgogoro huo ambapo amesisitiza juhudi za kukomesha mapigano na kuzijumuisha pande zinazopingana katika majadiliano.

Bwana Jeremic amesema huu ni wakati muhimu wa kushinikiza mkutano wa amani Syria akifafanua kwamba matokeo yanayofikiwa kwa njia ya majadiliano ya kisiasa ndio njia pekee ya kukomesaha umwagaji damu na kuzitaka nchi wanachama wa Umoja huo kutekeleza lengo hilo.

Amesema matumizi ya kijeshi yataendeleza mateso kwa raia wa Syria na kukuza mgogoro. Pia Rais huyo wa baraza kuu la UM amerejelea msimamo wa umoja huo ya kwamba ikiwa tuhuma dhidi ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria zitathibika, nchi wanachama ziungane katika kuendeleza jukumu muafaka katika kuheshimu sheria za kimataifa ikiwa ni pamoja na umuhimu wa jukumu la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa katika makataba wake.