Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika iko tayari kuanzisha mfumo wa kidigital wa televisheni:

Afrika iko tayari kuanzisha mfumo wa kidigital wa televisheni:

Nchi 47 za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara zimeafikiana masafa ya ushirikiano kwa ajili ya kuhamia kwenye mfumo wa digital wa televisheni ifikapo 2015. Flora Nducha na taarifa zaidi

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Majadiliano ya mipango ya kitaifa ya utekelezaji wa kuhamia mfumo wa kidigital Afrika yamefanikiwa na kuthibitishwa kwa kujiwekea hadi Juni 2015 kutekelezwa kwa masafa ya UHF na Juni 2020 masafa ya VHF katika nchi 33. Malengo ya hatua hii yaliwekwa mwaka 2006 na mkutano ulioandaliwa na ITU.

Hatua hii kubwa inalifanya bara la Afrika kuwa ni la kwanza kwa mwaka 2015 kuwa na masafa huru ya kuhamia mfumo wa digital wa televisheni. Maamuzi ya mkutano wa kimataifa wa mawasiliano mwaka 2012 wa kusaidia upatikanaji wa masafa huru kwenda kwenye huduma ya simu yataanza kutekelezwa rasmi mara baada ya mkutano wa kimataifa wa mawasiliano mwaka 2015.

Katibu mkuu wa ITU Hamadoun I. Toure ameshukuru kwa ushirikiano wa hali ya juu katika mchakato mzima ulioonyeshwa na jumuiya ya mawasiliano ya Afrika ATU na katibu mkuu wake bwana Abdoulkarim Soumaila.Amesema lengo kubwa ni kuziwezesha nchi za Afrika kuwa na masafa huru ya digital na hivyo kutopitwa saana na maendeleo ya teknolojia ya kisasa.