Wavamizi wa eneo la wakimbizi huko Uganda wafurushwa

4 Septemba 2013

Serikali ya Uganda imeanza kuwafurusha zaidi ya watu elfu hamsini walioingilia ardhi ya Kambi ya wakimbizi ya Kyangwali. Zoezi hilo lina lengo la kupata makazi kwa maelfu wakimbizi ya wanaoendelea kuingia nchini humo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC). John Kibego wa radio washirika ya Spice FM, anaripoti kutoka Hoima, Uganda.

(Tarifa ya Kibego)

Wanofurushwa wako katika vijiji 13 kwenye ardhi enye ukibwa wa kilomita 36 mraba, sehehu ya ardhi ya kambi ya wakimbizi ya Kyangwali, enye ukibwa wa kilomita 117 mraba. Idadi kubwa ya watu hao ni wahamiaji kutoka sehemu mbali mbali nchini na wengine ni wenye asili ya Rwanda. Waliingilia ardhi hiyo katika muongo uliopita, kujijengea makazi na wamekuwa wakitekeleza shughuli za kuichumi kama vile klimo, na uchomaji makaa. Douglous Asiimwe, ni afisa mwandamizi wa kutetea wakimbizi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

(Sauti ya Douglous Asiimwe)

Wakimbizi kutoka DRC, wamekuwa wakiingia kwa wingi nchin Uganda siku za hivi karibuni kufuatia kuongezeka kwa makabiliano kati ya jeshi la serikali ya nchi hiyo na wanamgambo wa M23 katika jimbo la Kivu ya Kaskazini. Wengi wao wameletwa wilayani Hoima katika kambi hiyo ya Kyangwali, kambi iliyo kubwa kuliko zote humu nchini.