Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya chakula nchini Zimbabwe yazidi kuzorota: WFP

Hali ya chakula nchini Zimbabwe yazidi kuzorota: WFP

(Taarifa ya Grace)

Katika kukabiliana na hali hiyo ya uhaba wa chakula Zimbambwe, WFP na washirika wake watagawa nafaka pamoja na mafuta ya kupikia. Pia mgao wa fedha utatolewa kwenye maeneo fulani kama moja ya njia ya kuhakikisha kuendelea kuhudumu kwa masoko. Huduma hiyo inatarajiwa kuendeshwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu hadi msimu wa mavuno mwezi Machi mwaka ujao. Elisabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)

"Hali ya usalama wa chakula inadorora na ni mbaya zaidi kuwahi kushudiwa tangu 2009. Kukosekana kwa usalama wa chakula nchini Zimbabwe kumesababishwa na mambo kadha ikiwemo, hali ya hewa, kupanda kwa gharama ya maisha, na kukosekana kwa mbolea na mbegu na uwezekano wa ongezeko la bei za vyakula kwa sababu ya mavuno duni. Tunashirikiana na serikali kuimarisha ustahimili wa jamii, na kwa sasa tunasubiri msimu wa mavuno ni lazima tuwapatie msaada wa chakula"