Mashauriano yafanyika Arusha katika jitihada za kutafuta amani ya kudumu Darfur, Sudan

30 Agosti 2013

Jimbo la Darfur nchini Sudan limekuwa na mzozo kwa miaka kumi sasa kati ya serikali na vikundi vya upinzani. Mzozo huo umesababisha mapigano ya mara kwa mara kwa misingi tofauti ikiwemo ile ya kikabila, kiuchumi na kisiasa. Mzozo huo ulisababisha kupitishwa kwa makubaliano ya amani ya Dohakwa ajili ya Darfurya mwaka 2011.

Hata hivyo baadhi ya vikundi vikubwa ikiwemo kile cha Minni Minnawi  havikusaini makubaliano hayo na hivyo kuendelea kuweka amani ya Darfur mashakani. Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID  ukapendekeza mashaurianokama njia ya kushawishi vikundi hivyo kuweza kujiunga na makubaliano. Mashauriano hayo yamefanyikaArusha,Tanzania kuanzia tarehe 22 hadi 27 mwezi Agosti mwaka 2013. Je nini kiliafikiwa? Je kuna matumaini ya amani? Assumpta Massoi wa Idhaa hii alizungumza na Kaimu Mkuu wa kikosi cha UNAMID Luteni Jenerali Wynnjones Kisamba na hapa anaanza kwa kuelezea kile kilichowapeleka Arusha.

 (PCKG YA ASSUMPTA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter