Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuheshimu haki za binadamu ni muhimu kwa utulivu DRC:Pansieri

Kuheshimu haki za binadamu ni muhimu kwa utulivu DRC:Pansieri

Vita dhidi ya ukwepaji sheria na kuheshimu haki za binadamu ni muhimu kwa kurejesha utulivu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema naibu kamisha mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Flavia Pansieri , wakati akikamilisha ziara yake ya siku saba nchini humo. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Bi Pansieri amesema ilikuwa muhimu kufanya ziara hiro Congo sio tuu kwa sababu ya hali mbaya ya haki za binadamu lakini pia kusisitiza msimamo wa ofisi yake wa kuisaidia serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na watu wake kukabiliana na changamoto nyingi zinazowakabili kuhusu suala la haki za binadamu.

Naibu kamishina huyo alizuru Goma Agost 22 na 23 na kulaani vikali mashambulizi dhidi ya raia akisema yanakwenda kinyume na sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Ameongeza kuwa watu wa Kivu Kaskazini na Ituri wamemuelezea masaibu yanayowakabili kila siku za maisha yao na kujionea upungufu wa taasisi za serikali na kutozingatiwa kwa maadili. Amesema pia amesikitishwa na kiwango cha ukatikli wa kingono unaofanywa na makundi ya watu wenye silaha na majeshi ya ulinzi na usalama. Alizuru pia maenmeo ya Kitchanga huko Masisi na pia Bunia ambako alishuhudia hali mbaya ya wafungwa. Amemalizia kwa kuwaahidi watu wa Congo na aserikali kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwasaidia ili kurejesha amani na utulivu.