Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo au amani ya muda havina tija, viongozi sikilizeni wananchi wenu: Ban

Maendeleo au amani ya muda havina tija, viongozi sikilizeni wananchi wenu: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa mhadhara kuhusu uhuru kwenye Chuo Kikuu cha Leiden huko The Hague, Uholanzi na kueleza bayana kuwa harakati zozote za kuweka amani au maendeleo ya muda hazina tija, kwani mambo hayo mawili yanapaswa kuwa endelevu. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Majira ya asubuhi kwa saa za Uholanzi, jopo la wahadhiri wa chuo kikuu chaLeidenlikimwongoza Katibu Mkuu Ban Ki-Moon kuingia katika ukumbi tayari kutoa mhadhara wa Nne kuhusu Uhuru. Ndani ya ukumbi wageni waalikwa wakisubiri kwa hamu kusikiliza kile atakachosema wakati huu ambapo macho na masikio yameelekezwa Mashariki ya Kati hususanSyria, ambako yadaiwa matumizi ya silaha za kemikali. Bwana Ban akaanza kwa kuzungumzia kuwa uhuru wa dhati  unajengwa katika misingi mikuu mitatu ambayo ni maendeleo ya kweli yanayotoa hakikisho la mtu kutosheka, amani na usalama vinavyofanya mtu asiwe na woga au hofu ya kuishi pamoja na haki za binadamu. Lakini la msingi hivyo vitu visiwe vya muda bali endelevu…..

(Sauti ya Ban)

“Huwezi kuwa na amani bila maendeleo, huwezi kuwa na  maendeleo bila amani. Inaweza ikawepo amani ya muda lakini  hilo si endelevu. Yanaweza kuwepo maendeleo ya muda. Bila kuwepo kwa usalama wa kisiasa huwezi kufanya biashara, na pia vyote haviwezi kufanikiwa bila kuheshimu haki za binadamu na utawala wa kisheria.”

Katibu Mkuu akaenda mbali zaidi na kusema kuwa kuhifadhi uhuru si kazi ndogo, kwani kuna gharama yake na yahitaji uwekezaji. Mathalani wananchi wapatiwe fursa na pahali pa kutoa madukudukuyaohivyo akatoa ushauri kwa viongozi..

(Sauti ya Ban)

 

Sikiliza, sikiliza, hili ni neno moja tu limekuwepo tangu kuanza kwa mataifa ya kiarabu, nimekuwa nawasihi viongozi sikiliza kwa makini matarajio na hofu ya wananchi wenu hata matatizo yo. Kama hamtawasikiliza, nini kitatokea, mtawasikia mitaani, kwenye viwanja au mbaya zaidi vitani. Tumeshuhudia kwa miaka kadhaa sasa.. angalia Syria, tangu viongozi wa Syria wagome kuwasikiliza wananchi wao, sasa kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe, Misri, Libya, Tunisia na kwingineko.”