Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM amekwenda Cairo “kusikiliza”

Mjumbe wa UM amekwenda Cairo “kusikiliza”

Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa siku ya jumatano alikuwa nchini Misri kwa ajili ya kuwasikiliza raia wake kabla ya kuchukua hatua za kushughulikia mzozo unaendelea sasa.

Jeffrey Feltman ambaye ni msaidizi wa Katibu Mkuu katika masula ya siasa amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Nabil Fahmy na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiarabu Nabil El-Araby.

Bwana Feltman alisema kuwa mazungumzo yake na Bwana El-Araby yaliegemea zaidi namna ya kuwa na ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu.

Pia walijadiliana namna ya kuwa na suluhu ya kisiasa kwa mzozo wa Syria, mazungumzo ya uletaji amani baina ya Israel na Palestina na suala la Yemen,, kuangalia Umoja wa Mataifa unavyoweza kujiingiza.

Eduardo del Buey ni msemaji wa Umoja wa Mataifa.