Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wa wakimbizi wa Syria waingia Iraq:UNHCR

Maelfu wa wakimbizi wa Syria waingia Iraq:UNHCR

Mkuu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR anasema kuwa maelfu ya wasyria walivuka mpaka na kuingia kaskazini mwa Iraq siku ya Alhamisi, kukitajwa kuwa kuhama kwa ghafla kunakowahusisha watu wengi. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Jason)

Maafisa wa UNHCR walio nje wanasema kuwa watu wengi wanahama wakitumia daraja mpya iliyojengwa katika eneo la Pashakhabour. Kundi la kwanza la wasyria likiwa ni la watu 750 waliovuka daraja hiyo masaa ya mchana. Baadaye jioni kundi lingine la kati ya watu 5000 na 7000 lilifuatia. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(Sauti ya Adrian)

”Wengi wa wanaowasili sasa ni familia hususan kutoka Aleppo . Kiini cha kuhama huku kwa ghafla hakijulikani kwa UNHCR kwa sasa. Wasyria wengine wamekuwa wakisubiri karibu na mto Tigris kwa siku mbili au tatu.”

Katika upande mwingine UNHCR inasema kuwa wiki hii imeanza kuwahamisha wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo waliovuka na kuingia mashariki wa Uganda tarehe 11 ,mwezi Julai kufuatia mashambulizi kutoka kwa kundi moja la waasi mashariki mwa DRC.