Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki za binadamu bado unaendelea CAR: Šimonović

Ukiukwaji wa haki za binadamu bado unaendelea CAR: Šimonović

Kati ya Disemba 2012 na Machi mwaka 2013, vikosi vya waasi wa Seleka na vikosi vya serikali ya zamani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati vilitekeleza ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa za haki za binadamu na sheria za kibinadamu, ingawa uhalifu ulotekelezwa na waasi wa Seleka ulikuwa mwingi zaidi.

Hayo yamesemwa na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu Haki za Binadamu, Ivan Šimonović, katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo limekutana kujadilia hali katika Jamhuri ya Afrika ya Kati hii leo.

Bwana Šimonović  amesema, kufuatia kunyakuliwa kwa mamlaka na waasi wa Seleka, ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na waasi hao umeendelea hata kufikia sasa.

 "Ukiukwaji ambao umetekelezwa unajumuisha mauaji kinyume na sheria, mauaji kiholela, kulazimu watu kutoweka, watu kukamatwa na kutiwa rumande kiholela, utesaji, ukatili wa kiingono na kijinsia, uhalifu dhidi ya watoto, yakiwemo mauaji, ubakaji, kuwasajili katika jeshi na kuwatumia kama ngao za binadamu, pamoja na kuharibu na kupora mali za kibinafsi na za umma, zikiwemo hospitali, shule, majengo ya serikali, na ofisi za Umoja wa Mataifa na nyingine za kimataifa."

Bwana Šimonović  amesema waandishi wa habari na wanaharakati wa umma ambao wamejaribu kukosoa ukiukwaji huo wameshambuliwa. Amesema kumekuwa na uharibifu wa daftari za umma,kamazile za watoto wanaozaliwa na zile za magereza. Ameongeza kuwa ingawa hali ya usalama katika mji mkuuBanguiimetengamaa kidogo, kwingineko nchini hamna utaratibu wowote wa kisheria, na kwamba watu wanaishi kwa hofu kubwa.