Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aitaka Hamas kuacha kutekeleza hukumu ya kifo

Pillay aitaka Hamas kuacha kutekeleza hukumu ya kifo

Kamishna mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay  ameutaka utawala wa kundi la Hamas kwenye Ukanda wa Gaza kuachana na mipango ya kuwanyonga watu wanaokabiliwa na hukumu ya kifo kwa kuwa ni kinyume na sheria kimataifa kuhusu haki za binadamu.Mkuu wa sheria kwenye Ukanda wa Gaza alitoa matangazo kadha wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan  kuwa baada ya sherehe za Eid al- Fitr shughuli ya kuwanyonga watu wanokabiliwa na hukumu ya kifo itafanyika. Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema ana wasiwasi  kuwa huenda watu hao wakanyongwa siku zinazokuja ambapo ametoa wito kwa utawala katika eneo hilo  kuacha kutekeleza hukumu hizo.

Bi Pillay amesema kuwa sheria za kibinadamu za kimataifa zinanahitaji kufuatwa  kuambatana na viwango vya kimataifa wakati kunapotolewa hukumu ya kifo. Pia anaelezea wasiwasi kuhusu jinsi hukumu za kifo zinavyotolewa kwenye makahama za kijeshi na kiraia kwenye Ukanda wa Gaza. Elizabeth Throssell ni msemaji wa tume ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa.

 (Sauti ya Elizabeth)