Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam waitaka Israel “iache kumnyanyasa mtetezi wa haki za binadamu Issa Amro”

Wataalam waitaka Israel “iache kumnyanyasa mtetezi wa haki za binadamu Issa Amro”

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Kundi la wataalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu limeelezea kusikitishwa na madai ya vitisho na unyanyasaji unaotekelezwa na vyombo vya dola vya Israel dhidi ya Issa Amro, mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu za Wapalestina.

 Bwana Amro alikamatwa na kutiwa rumande mara 20 mnamo mwaka 2012, na mara 6 kufikia sasa katika mwaka huu 2013, ingawa hakuwahi kushiriki ghasia, wala kushtakiwa kwa makosa yoyote. Bwana Amro ni mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la vijana wanaopinga kuwepo kwa makazi ya Waisraeli kwenye maeneo ya Wapalestina yalokaliwa.

Mtaalam maalum kuhusu hali ya haki za binadamu kwenye maeneo hayo, Richard Falk ametoa wito kwa serikali ya Israel kuhakikisha kuwa madai yote ya utesaji na udhalilishaji wa Wapalestina wanaozuiliwa na vyombo vya dola yanachunguzwa kwa njia ilo wazi na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mtaalam huru kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu, Bi Margaret Sekaggya amesema kuendeleza vitendo vya unyanyasaji na vitisho dhidi ya Bwana Amro na watetezi wengine wa haki za binadamu hakukubaliki. Naye Frank La Rue, ambaye anahusika na uhuru wa kujieleza amesema vitisho vinavyotokana na kukamatwa kwa watu kiholela huenda vikawanyamazisha wale ambao hutoa habari muhimu kuhusu hali halisi ilivyo.