Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kitabu cha anuani kuhusu waathirika wa biashara ya binadamu kuzinduliwa Tanzania:IOM

Kitabu cha anuani kuhusu waathirika wa biashara ya binadamu kuzinduliwa Tanzania:IOM

Kitabu maalum cha anuani, ruznama ,za mashirika ya kusaidia kupinga biashara haramu ya usafirishajii wa binadamu kilichochapishwa na shirika la kimataifa la uhamiaji , IOM, kinazinduliwa August 5 mjini Dar es salaam.Ruznama hiyo inatoa maelezo na anuani za mashirika ya kinadamu ya serikali, asasi za kiraia, na mashirika ya kimataifa katika ukanda wa Tanzania ambayo yanaweza kusaidia waathirika wa usafirishaji haramu. Misaada hii inahusisha malazi, msaada wa kisaikolojia, matibabu, misaadaya kisheria na mafunzo ya ufundi stadi.

Kwa mujibu wa IOM Ruznama hii ambayo itatumika kama chombo cha kuratibu huduma miongoni mwa mashirika ili kutoa ulinzi stahiki kwa waathirika nchini humo ni matokeo ya ripoti ya serikali ya Marekani kuhusu biashara ya binadamu na utafiti wa IOM. Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe anafafanua.

(SAUTI JUMBE)

Visa vya biashara haramu ya binadamu wanaosafirishwa ili kutumiwa katika biashara ya ngono pia vimeripotiwa katika mpaka kati ya Tanzania na Kenya.