Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa kuomba hifadhi Ukraine unahitaji kuimarishwa:UNHCR

Mfumo wa kuomba hifadhi Ukraine unahitaji kuimarishwa:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema mfumo wa kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini Ukraine bado unahitaji kuimarishwa.UNHCR na serilkali ya Ukraine wanahitaji kutoa ulinzi bora zaidi dhidi ya waomba hifadhi ili wasirejeshwe kwa nguvu na pia kuimarisha mchakato wa kusikiliza kesi za kuomba hifadhi uwe unaoeleweka na ulio na usawa.

Kutokana na hofu hiyo shirika la UNHCR linazishauri nchi nyingine pia zisiwarejeshe waoomba hifadhi kutoka nchini Ukraine kwa wakati huu.