Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

USAID yatoa msaada wa chakula kwa waathirika wa ukame Djibouti:WFP

USAID yatoa msaada wa chakula kwa waathirika wa ukame Djibouti:WFP

Ofisi ya chakula kwa ajili ya amani ya shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa USAID imetoa fungu la kwanza la mchango wake wa dola mulioni 4 za mwaka 2013 kwa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ajili ya kuisaidia serikali ya Djibouti. Grace Kaneiya anaripoti.(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Msaada huo wa dharura unalenga kuwasaidia haswa watu waishio vijijini ambao wanakabiliwa na uhaba wa chakula hali inayosababishwa na ukame. Msaada huo unaogezea hifadhi ya nafaka na mafuta ya kupikia ya Shirika la WFP . Mchango huu utakuwa muhimu katika kuyaafikia mahitaji ya kibinadamu watu maskini walio vijijini nchiniDjiboutiambao wametatizwa na ukame kwa miaka mingi. Serikali ya Marekani inashirikiana kwa karibu na serikali yaDjiboutikuweza kutatua suala la usalama wa chakula kwa njia nyingi. Katika vita dhidi ya utapiamlo Shirika la USAID limeisaidia serikali yaDjiboutikatika kupunguza vifo vya watoto walio  kwenye hali mbaya ya utapiamlo kutoka asilimia 20 mwaka 2006 hadi asilimia 0.2 mwaka 2012. Mipango ya WFP  inayoungwa mkono na michango  ya mara kwa mara kutoka kwa serikali ya Marekani inawasaidia watu maskini nchiniDjiboutikujikwamua kutoka kwenye umaskini  na kuwahakikishia maisha bora ya baadaye.