UNHCR yazitaka nchi majirani kufungua mipaka kuwapokea wakimbizi wa Syria

16 Julai 2013

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa wakimbizi António Guterres amezitaka nchi kufungua mipaka kwa ajili ya wakimbizi wa Sryia kuvuka huku pia akonya hatua za haraka lazima zichukuliwe kupunguza hatari ya ukosefu wa amani kwa nchi jirani.

Akiwahutubia wajumbe wa baraza la usalama kwa njia ya video kutoka mjini Geneva , Gutteres ametaka nchi zote katika ukanda huo kufungua mipaka na kuwapokea wakimbizi hao wanaotafuta hifadhi na kusisitiza kwamba mshikamano miongoni mwa nchi jirani, utoaji makazi, fursa za kuwapokea na ubinadamu ni muhimu katika kutimiza hatua hiyo.

Bwana Guterres ameelezea wasiwasi wake wa kuendelea kwa mapigano nchini Syria kutokana na matarajioa ya suluhisho la kisiasa kufifia na kuonya pia kuhusu kukosekana kwa utulivu kwa nchi zinazohifadhi wakimbizi wa nchi hiyo ambapo kumekuwa na mfumuko wa bei unaoweza kuendelea ikiwa jumuiya ya kimataifa haitachukua hatua za kusaidia.

Kamishana Mkuu huyo wa Umoja Matifa wa wakimbizi amesema anaelewa changamoto ambazo nchi ya Misri inapitia lakini akasema ana matumaini wataendeleza ukarimu wao kwa wakimbuzi wa Syria kama amavyo wamekuwa wakifanya tangu kuzuka kwa mapigano.