Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe maalum wa UM apongeza kuondolewa kikosi cha kulinda mpaka nchini Myanmar

Mjumbe maalum wa UM apongeza kuondolewa kikosi cha kulinda mpaka nchini Myanmar

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kibinadamu nchini Myanmar Tomas Ojea Quintana ameunga mkono kuondolewa kwa kikosi cha kulinda mpaka kinachofahamika kama Nasaka kinachoendesha shughuli zake kwenye jimbo la Rakhine.Mjumbe huyo maaalum ametaka utawala wa Myanmar kufanya uchunguzi na kuwachukua wale waliohusika kwenye ukiukaji wa haki za binadamu. Tomas Ojea Quintana amesema kuwa amepokea madai ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaokihusisha kikosi hicho cha Nasaka hasa dhidi ya jamii ya watu wa Rohingya yakiwemo mauaji, kukamatwa bila ya hatia, kuzuiliwa na kuteswa.

Kwenye ripoti yake ya mwezi Machi kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjumbe huyo alitoa pendekezo akitaka kuondolewa kwa kikosi hicho  kwenye jimbo la Rakhine na kukifanyia mabadiliko.