Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali nchini Misri bado ni tete

Hali nchini Misri bado ni tete

Taarifa kutoka nchini Misri zinasema takriban watu 42 wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsy walikua wamekusanyika na wakiamini kuwa Rais wao anashikiliwa mahali hapo, Watu wengine 300 wamejeruhiwa.

Kundi la Muslim  Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale wote linaowaita waporaji wa uhuru na demokrasia. Kundi hilo la Muslim Brotherhood linalaumu jeshi la nchi hiyo kwa mauaji ya raia wake.