Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yazidi kuzua madhara makubwa kwa raia kwenye mji wa Kismayo

Mapigano yazidi kuzua madhara makubwa kwa raia kwenye mji wa Kismayo

Mapigano makali ya hivi majuzi kati ya makundi hasimu kwenye mji ulio pwani ya Somalia wa Kismayo yanaendelea kuwaathiri raia na makundi ya kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo la Juba. Watu wote waliojeruhiwa kwenye mapigano hayo mwezi wa Juni ni watu 314 wakiwemo wanawake 15 na watoto 5 walio chini ya miaka mitano. Jumla ya watu 71 waliuawa 11 wakifa wakiwa hospitalini.

Taarifa zaid na Grece Kaneiya

Shirika la afya duniani WHO limepokea ripoti zinazosema kuwa watu wengine 60 waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini mjini Mogadishu huku 51 wakipelekwa Galkayo kwa matibabu zaidi. Idadi ya waliokufa kabla ya kufikishwa hosptalini inakisiwa kuwa ya juu hata kama bado haijathibitishwa. Wengi walipata majeraha ya kichwa na kifua huku zaidi ya waathiriwa 40 wakifanyiwa upasuaji. Tangu mwezi Januari hadi Juni mwaka huu majeraha 661 yatokanayo na silaha yalitibiwa mjini Kismayo . Kismyao unasalia kuwa mji hatari huku mapigamno kati ya pande hasimu yakizidi kuchacha pamoja na matukio mengine kama mabomu ya ardhini na yale ya kutupwa kwa mikono. Mizozo imesabisia kuhama kwa watu wengi jambo ambalo limesamabisha watu hao kukosa huduma za afya na kuchangia kuwepo kwa mikurupuko ya magonjwa yanayoambukiza yakiwemo kipindupindu. Hali hiyo pia imechagia kucheleweshwa kwa kampeni ya utoaji wa chanjo dhidi ya ujonjwa wa polio.