Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu inafuatilia hali nchini Misri:

Ofisi ya haki za binadamu inafuatilia hali nchini Misri:

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa uimesema inafuatilia kwa karibu hali tete inayoendelea nchini Misri na kuwaahidi watu wa taifa hilo kuwa waashikamana nao na wako tayari kuwasaidia. Flora Nducha na taarifa kamili(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Kwa mujibu wa ofisi hiyo tangu kuzuka kwa maandamano mara ya kwanza Januari 2011 nchini humo kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pilay amekuwa akiunga mkono haki ya uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa watu wa Misri, huku akizitolea wito pande zote kutatua tofauti zao na kujizuia kuendeleza machafuko.

Ofisi hiyo imeitaka serikali ya Misri kuendelea kufanya kila juhudi kulinda haki za raia wake za kujihusisha na maandamano ya amani. Pia imelaani vifo vya watu kadhaa vilivyotokea Jumapili na kusistiza kwamba kila aliyehusika na mashambulizi dhidi ya walioandamana kwa amani na wale watakaobainika walitumia nguvu kupita kiasi lazima wawajibishwe. Pia imezitaka pande zote kujihusisha na mazungumzo kupata suluhu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

"Tunazitaka pande zote za kisiasa na makundi ya kijamii kujihusisha haraka na mazungumzo ya kitaifa ili kupata suluhu na mgogoro wa kisiasa na kuzuia kuendelea kwa machafuko . Tuna mtolea wito Rais wa Misri kusikiliza madai na matakwa ya watu wa Misri yaliyoelezwa wakati wa maandamano katika siku chache zilizopita na kushughulikia masuala muhimu yaliyotajwa na upande wa upinzani na makundi ya kiraia katika miezi ya karibuni, pamoja na kupata funzo ya yale yaliyojfanyika siku za nyuma katika hali hii tete"

Pia ofisi hiyo ya haki za binadamu imekaribisha hakikisho lililotolewa na mashirika polisi na jeshi kwamba hakuna hatuia zozote zitakazochukuliwa zitakazosababisha matumizi ya nguvu dhidi ya wanaoandamana kwa amani.