Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM imeanza kufikisha msaada kwa wakimbizi wa Syria waioko Lebanon

IOM imeanza kufikisha msaada kwa wakimbizi wa Syria waioko Lebanon

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza kufikisha msaada kwa wakimbizi wa Syria 26,000 familia zinazowahifadhi na familia za Kilebanon zinazorejea huko Kusini mwa Lebanon.Operesheni za IOM zilisitishwa kwa muda mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na mapigano ya Jumapili kati ya jeshi la serikali ya Lebanon na waasi wanaomuunga mkono kiongozi wa kidini Salafi , lakini Jumatano IOM imeaanza tena kupeleka msaada kama anavyoarifu Jumbe Omari Jumbe afisa wa IOM.

 (SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

Wakati huo huo chama cha mabunge duniani, IPU kimetoa wito kwa kupatiwa suluhu ya haraka ya kisiasa kwenye mzozo wa Syria.

Kauli hiyo yafuatia ziara ya ujumbe wa chama hicho kwenye kambi za wakimbizi wa Syria nchini Jordan ambapo walishuhudia madhila kwa wakimbizi na athari kwa nchi zinazowahifadhi.