Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi mpya Burkina Faso kuwezesha nchi hiyo kukabiliana na utapiamlo

Mradi mpya Burkina Faso kuwezesha nchi hiyo kukabiliana na utapiamlo

Kufuatia uhaba wa chakula hukoBurkina Fasomwaka 2012, shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP nchini humo limeanzisha mradi mpya wa kuchagiza jamii kuibuka katika mgogoro huo wa chakula na hatimaye kuweza kukabiliana na halikamahiyo baadaye iwapo itatokea huku pia ikipunguza utapiamlo. Ripoti ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi.(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Burkina Fasoimeshuhudia mavuno mazuri mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mavuno ya nafaka kutoka mwaka 2012 na 2013 yaliongezeka kwa asilimia 30 yakilinganishwa na ya mwaka 2011 na 2012.

Kutokana na hali ya kiangazi iliyoshuhudiwa  kati ya mwaka 2011 na 2012 bado taifa hilo halijajikwamua kutoka kwenye janga la njaa huku watu milioni 1.8 nchini Burikana Faso wakikabiliwa na uhaba wa chakula. Familia nyingi zinakabiliwa na changamoto za kupata chakula .

Mwaka 2012 viwango vya utapiamlo vilipita vile vinavyowekwa na Shirika la afya dunianii WHO huku viwango vya watoto wasiokua vikifikia asilimia 33. Kwa sasa shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanzisha oparesheni ya kukabiliana na utapiamlo kwenye maeneo yaliyoathiriwa zaidi. Opareshini hiyo itaendeshwa kwenye maeneo 10 kati ya maeneo 13 ambapo itatoa chakula maalum na tiba kwa watoto  walio kati ya miezi 6 na 59 walio na utapiamlo.