Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zamulikwa

Operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zamulikwa

MjiniNew York, Marekani hii leo Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepokea taarifa za utendaji wa vikosi vya ulinzi wa amani vya umoja huo, zikiwasilishwa na makamanda wa vikosi hivyo ambao wamekuwa wakikutana hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Joshua Mmali na ripoti kamili.

(TAARIFA YA JOSHUA MMALI)

Mada kuu ambazo zimejadiliwa kwenye Baraza la Usalama ni matumizi ya teknolojia ya kisasa katika utekelezaji majukumu ya ulinzi wa amani, ukaguzi na tathmini za mafunzo ya vikosi vya kulinda usalama kabla ya kutumwa kutekeleza majukumuyao, pamoja na ushirikiano baina ya jumbe za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

Barazahilolimesikiliza taarifa za  makamanda watatu wa vikosi vya kulinda amani, ambapo Kamanda wa kikosi cha kuweka utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, MONUSCO, Luteni Jenerali Carlos Alberto Santos Cruz, ambaye amesema…

Makamanda wengine waliotoa taarifa ni kamanda wa kikosi cha kulinda amani nchini Cote d’Ivoire, UNOCI, Meja Jenerali Muhammad Iqbal Asi, na Kamanda wa Ujumbe wa kulinda amani nchini Liberia, UNMIL, Meja Jenerali Leonard Muriuki Ngondi.