UNRWA yalaani mauaji ya wakimbizi sita wa kipalestina huko Damascus

21 Juni 2013

Masahibu yanayokumba wakimbizi wa Syria ni zaidi ya uhaba wa chakula ambapo ripoti zinasema kuwa wakimbizi sita wa kipalestina wameuawa  nje kidogo ya mji mkuu waSyria,Damascus baada ya makombora yapatayo matatu kutua katika kambi ya wakimbizi wa kipalestina ya Khan Eshieh. Hadi sasa haijafahamika nani aliyerusha makombora hayo. George Njogopa na maelezo zaidi.(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kumekuwa na uharibifu mkubwa ikiwemo kushambuliwa kwa maskani moja ya UNRWA ambayo ndani yake kulikuwa na shule iliyokuwa ikiwachukua kiasi cha watu 260 ambao hawana makazi.

Katika tukiohilo, wakimbizi watano wa Kipalestina ikiwemo watoto wawili na wanawake wawili waliuwawa wakiwa ndani ya shule hiyo na wengine kiasi cha watu saba wanaripotiwa kujeruhiwa vibaya.Watu hao waliojeruhiwa ni pamoja na afisa mmoja wa UNRWA.

Baadhi ya majeruhi kwenye tukiohilowanaendelea kupata matibabu.

 

Kunaripoti ya kuuwawa kwa mkimbizi mwingine aliyekuwa kwenye kambi nyingine.

UNRWA imelaani vikali shambulizihiloililoliita la kinyama na linalowatisha raia.

===============

Katika hatua nyingine mwili wa raia wa Kenya Rita Muchucha aliyeuawa kwenye shambulio la kigaidi hukoSomalia siku ya Jumatatu umewasili Kenyakwa mazishi. Bi. Muchucha alikuwa akifanya kazi kitengo cha shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchiniSomalia.