Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lataka Libya isaidiwe kuimarisha mifumo ya usalama na sheria

Baraza la Usalama lataka Libya isaidiwe kuimarisha mifumo ya usalama na sheria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limetoa wito kwa jamii ya kimataifa iendelee kuisaidia serikali ya Libya katika juhudi zake za kuongeza uwezo wa taasisi zake za kiusalama na kisheria ili ili iweze kutamatisha kipindi cha mpito na kukaribisha demokrasia kamilifu, ukuaji wa uchumi, na utoaji huduma za umma.

Haya yamejiri baada ya Baraza hilo kupokea ripoti ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL, Tarek Mitri, mnamo Jumanne, Juni 18, ambayo ilitaja hatua za maendeleo zilizopigwa chini ya Waziri Mkuu Ali Zeidan, pamoja na changamoto zilizopo bado.

Wanachama wa Baraza hilo wameelezea masikitiko yao kufuatia matukio ya ghasia Benghazi, ambayo yalisababisha vifo vya watu wengi, na kutoa mwito kwa raia wa Libya kuunga mkono taasisi zao halali za umma na kijeshi.