Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi izingatie viwango vya kimataifa vya sheria za habari: UM

Burundi izingatie viwango vya kimataifa vya sheria za habari: UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeitaka serikali ya Burundi kupitia tena sheria yake mpya ya vyombo vya habari na kuzingatia viwango vya kimataifa. Kauli hiyo imefuatia Rais wa Burundi kutia saini sheria mpya ambayo inadaiwa itabana uhuru wa vyombo vya habari. Katika sheria hiyo waandishi wanatakiwa kueleza vyanzo vya habari, faini kwa makosa ya uandishi imeongezwa asilimia 200, waandishi wanatakiwa kuwa shahada ya chuo kikuu au ujuzi wa miaka 10. Rupert Colville ni msemajo wa ofisi ya haki za binadamu

(CLIP YA RUPERT COLVILLE)