Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha mazungumzo ya amani Myanmar.

Ban akaribisha mazungumzo ya amani Myanmar.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekaribisha makubaliano yaliyofikiwa jana kati ya seriakali ya Myanmar na shirika liitwalo Kachin Independence baada ya mkutano wao wa kwanza ndani ya nchi hiyo tangu kuzuka kwa mgogoro baina yao mwezi June mwaka 2011.

Mshauri maalum wa Katibu Mkuu, Vijay Nambiar alikuwa miongoni mwa waanaglizi katika mazungumzo hayo kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, pamoja na mwakilishi wa ubalozi wa China, na mwakilishi wa makundi mbalimbali ya makabila nchini Myanmar.

Bwana Ban katika taarifa yake, ameyaita makubalaino hayo yenye vipengele saba, mafanikio muhimu yatakyoweka msingi wa mchakato wa kweli wa maridhiano ya kaitaifa nchini humo.

Kadhalika Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amewapongeza viongozi wa pande zote kwa ujasiri na uvumilivu wao na kusema anatumaini makubaliano hayo yatawezesha kushughulikia mahitaji ya jimbo la Kachin.

Bwana Ban amesisitiza muendelezo wa uungwaji mkono kutoka Umoja wa Mataifa na mshauri wake maalum katika maeneo hayo, wanapoendelea kufanya kazi kukomesha mzozo na kuelekea katika mazungumzo ya kina yatakayoleta amani ya kudumu nchini Myanmar.