Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laongeza muda wa UNISFA Abyei

Baraza la Usalama laongeza muda wa UNISFA Abyei

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja wamepitisha azimio la kuongeza muda wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda usalama kwenye eneo la Abyei, UNISFA kwa muda wa miezi sita zaidi, kuanzia mwezi Juni. Muda wa Kikosi cha UNISFA kwenye eneo hilo ambalo limekuwa likizozaniwa kwa muda mrefu kati ya Sudan na Sudan Kusini ulitakiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Azimio hilo limepitishwa kufuatia ripoti ya Katibu Mkuu Ban Ki-moon ilotaja tishio la kiusalama linalotokana na kuendelea kuwepo makundi yenye silaha kwenye eneo salama la mpakani, ambako wanajeshi waliondolewa na hawapaswi kuwepo tena. Ripoti hiyo pia iliomba idadi ya kikosi cha UNISFA iongezewe kwa wanajeshi 1, 126 zaidi.

Akiongea baada ya kupitishwa azimio hilo, Mwakilishi wa Sudan Kusini kwenye Umoja wa Mataifa, Francis Deng amelipongeza azimio hilo

(Sauti ya Deng)

Vile vile, Mwakilishi wa Sudan kwenye Umoja wa Mataifa Daffa-Alla Elhag Ali Osman amefurahia uamuzi huo wa Baraza la Usalama

(Sauti ya Osman)