Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Aina ya ugonjwa usiodhibitika wa polio waendelea kusambaa kwenye pembe ya Afrika

Aina ya ugonjwa usiodhibitika wa polio waendelea kusambaa kwenye pembe ya Afrika

Eneo la pembe ya Afrika kwa sasa linakabiliana na aina ya ugonjwa wa polio usiothibitika kwa kifupi WPV1. Mtoto wa umri a miezi minne anaripotiwa kuonekana akiwa na dalili za ugonjwa huo na kulemaa karibu na kambi ya Dadaab nchini Kenya mnamo tarehe 30 mwezi Aprili mwaka huu.

(RIPOTI YA JASON NYKUNDI)

Utafiti kuhusu ugonjwa huu unaendelea. Ili kukabiliana na mkurupuko huo kampeni ya kwanza ya utoaji wa chanjo ikiwalenga watoto 440,000 ilingo’a nanga mwezi Mei mwaka huu nchini Somalia huku awamu ya pili ikipangwa kuanza tarehe 26 mwezi huu kwenye sehemu zilizoathirika nchini Kenya. Hatari kwa mataifa jirani ni ya juu kutokana na kuhama kwa watu wengi kwenye upembe wa Afrika . Kambi ya Dadaab ni makao kwa karibu wakimbizi 500,000 kutoka sehemu tofauti za pembe ya Afrika. Tahadhari ya kutaka kufanyika utafiti imetolewa kwa nchi zote katika pembe ya Afrika ya kutaka kufanyiwa uchunguzi visa vyote. Mwaka 2005 ugonjwa wa polio ulisambaa kutoka barani Afrika hadi nchini Yemen ambapo visa 700 vya ugonjwa huo viliripotiwa. Tangu wakati huo chanjo mpya za ugonjwa wa polio zimebuniwa ambazo zitazuia mikurupuko ya ugonjwa wa polio kwa muda mrefu.