Ugonjwa wa Novel Corona virus waripotiwa Tunisia

Ugonjwa wa Novel Corona virus waripotiwa Tunisia

Wizara ya afya nchini Tunisia imelipa makataa Shirika la afya duniani WHO kuhusu kuthibitishwa kupitia kwa mahabara visa vya ugonjwa wa novel Coronavirus. Alice Kariuki na taarifa zaidi.

RIPOTI YA ALICE

Visa viwili vilivyothibitishwa kupitia kwa mahabara ni cha mwanamme mwenye umri wa miaka 34 na mwanamke wa umri wa kiaka 35 ambao wote ni ndugu wote wakiwa na matatizo ya kupumua. Kutokana na utafiti ni kwamba baba yao mwenye umri wa miaka 66 aliugua siku tatu baada ya kurejea nyumbani kutoka nchini Qatar na Saudi Arabia mnamo tarehe 3 mwezi Mei mwaka huu kabla ya kulazwa hospitalini. Hata hivyo hali yake ilizidi kuwa mbaya na akaaga dunia mnamo tarehe 10 mwezi Mei mwaka 2013 . Nchini Saudi Arabia mgonjwa ambaye awali alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa chini ya uchunguzi kutokana na mkurupuko wa ugonjwa huo tangu mwezi Aprili mwaka huu ameaga dunia. Kote duniani tangia mwezi Septemba mwaka 2012 WHO imefahamishwa kuhusu jumla ya visa 43 vya ugonjwa huo na vifo 21