Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF kuanza kutoa chanjo ya dharura kukabili surua CAR

UNICEF kuanza kutoa chanjo ya dharura kukabili surua CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF pamoja na washirika wake linajiandaa kuanzisha kampeni ya dharura kwa ajili ya njanjo kukabili tishio la ugonjwa wa surua ambao ameripotiwa kuwakumba watoto kadhaa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.Vipimo vilivyofanywa mwezi April mwaka huu katika mji mkuu Bangui vimebaini watoto 8 wamekumbwa na ugonjwa huo.

Kampeni hiyo inatazamiwa kufanywa kuanzia May 22 hadi 26 mwaka huu ikilenga kuwafikia zaidi ya watoto 125,00 .

Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF

(Marixie Audio)