Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasyria milioni 8.3 wanahitaji msaada kuishi

Wasyria milioni 8.3 wanahitaji msaada kuishi

Karibu wasyria nusu milioni kwa sasa wanategemea misaada ya kibinadamu kuishi kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Alice Kariuki na taarifa kamili

(TAARIFA YA ALICE)

UNHCR inasema kuwa zaidi ya wasyria milioni 8.3 wanapokea misaada ya kibinadamu kama wakimbizi kwenye nchi majirani au kama wakimbizi wa ndani.

Shirika hilo linasema kuwa hali nchini Syria inazidi kuzorota wakati ghasia zinapoendelea na kuzuia kufikiwa wale wanaohitaji msaada. Panos Moumtzis ni mratibu wa UNHCR kwenye mzozo wa Syria.

“Tumefika mahala ambapo mahitaji ni ya juu kuliko misaada kughulikia mahitaji haya. Tuko mahala ambapo pamoja na mashirika ya kibinadamu tuko karibu kila wakati , tutafanya maamuzi kuhusu ni wapi tutapeleka misaada. Ni shughuli ya kuvunja moyo kuweza kuamua kati ya nchi na huduma tunazotoa na kuamua kilicho cha kuokoa maisha na nini kinachohitajika kwa dharura na kile kinachoweza kuwahudumia watu wengi wenye mahitaji kwa njia nzuri na mahitaji mengine kwenye maeneo hayo.”

Hata hivyo UNHCR inasema kuwa hakuna mkimbizi ambaye amewasili kwenye kambi ya Za’atari nchini Jordan kwa muda wa siku nne zilizopita, suala ambalo limezua hofu kuhusu usalama wa wasyria ambao wamehama makwao kwenye vijiji vilivyo mpakani na Jordan.