Pengo la huduma za afya kati ya nchi tajiri na maskini lapungua: WHO

15 Mei 2013

Shirika la afya duniani, WHO limetoa ripoti mpya kuhusu mwelekeo wa utoaji wa huduma za afya dhidi  ya Ukimwi, Kifua Kikuu na zile za uzazi na kubainisha kupungua kwa pengo la utoaji wa huduma hizo kati ya nchi maskini na zile tajiri. Ripoti hiyo inapigia chepuo harakati za kufikia malengo ya milenia kama kichocheo kikuukamaanavyoripoti Jason Nyakundi. (TAARIFA  YA JASON)Kupitia takwimu zake za kila za kiafya duniani WHO inasema kuwa jitihada za kuafikia malengo ya maendeleo ya milenia zimepunguza mwanya wa afya uliopo kati ya nchi matajiri na zile maskini. Inalinganisha hatua zilzopigwa na nchi zilizo na mifumo bora ya afya na zile zilzo na mifumo ya chini  kulingana na malengo ya maendeo ya milenia ya mwaka 1990 na miaka ishirikini baadaye. Inaonyesha kuwa nchi zilizo na asilimia 25 ambayo ni asilimia ya chini kiafya zimepiga hatua kubwa. Hatua zaidi pia zimepigwa katika kupunguza vifo vya watoto wakati wa kuzaliwa , kuboresha lishe na kupunguza vifo vinavyosabishwa na ugonjwa wa ukimwi , kifua kikuu na Malaria. Dr Ties Boema kutoka WHO  anasema kuwa hata kama mwanya wa  kiafya umepungua kati ya nchi maskini na zile tajiri duniani badohiloliko mbali na kutimizwa.

“ukiongalia upande wa vifo vya watoto, nchi kama Bangladesh, Bhutan, Laos Madagascar, Nepal, Rwanda, Senegal, Timor Leste zimetoka kwenye nchi za mwisho 25. Nchi ambazo hazijapiga hatua ni zile ambazo zimekuwa kwenye mizozo. Nchi kama Chad au Niger na Somalia. Kile tunachokiona ni kuwa ikiwa nchi zitatoka kwenye mizozo hatua zao zitakuwa kubwa kwa mfano kile ambacho Rwanda imefanya au kwa kiwango kidogo nchi kama vile Cambodia.”

WHO inasema kuwa vifo vinavyotokana na ugonjwa wa kifua kikuuu vimepungua kwa zaidi ya silimia 40 tangu mwaka 1990 na kuna ishara kwamba hii inaweza kutimia asilimia 50 ifikapo mwaka 2015.