Israel yaaswa dhidi ya ujenzi wa barabara ya njia sita Mashariki mwa Jerusalem

13 Mei 2013

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu Mashariki ya Kati Richard Falk Jumatatu ameionya Israel na kuitaka isitishe mara moja ujenzi wake wa barabara ya njia sita katika eneo la Beit Safafa Mashariki mwaJerusalem. Amesema maisha ya Wapalestina 9,300 yatasambaratishwa na ujenzi huokamautakamilika. Jason Nyakundi anaripoti(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Falk ambaye ametwikwa jukumu na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa la kuchunguza hali ya haki za binabamu kwenye utawala wa palestina tangu mwaka 1967 ameonya kuwa barabara hiyo kuu yenye barabara sita iliyo na urefu wa kilimota 1.5 itasababisha madhara makubwa kwa jamii kwa kufunga barabara zingine na maneo mengine yakiwemo shule, zahanati na meneo ya ibada.

Falk anasema kuwa wenyeji wa eneo la Beit Safafa hawakuombwa ushauri kabla ya kuanza kwa mradi huo. Mjumbe huyo amesema kuwa lengo la barabara hiyo ni kupanua makao hayo na ujenzi mwingine unaofanywa naIsraelmashariki mwaJerusalem.

Anasema kuwa mradi huo ulioanza mwaka 2012 ulipingwa kwenye mahakama moja mjiniJerusalemlakini kesi hiyo ilitupiliwa mbali sawia na kesi ilyowalishwa mahakamani iliyotupiliwa mbali mwezi Machi mwaka huu.