Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani Shambulizi la bomu Uturuki

Baraza la Usalama lalaani Shambulizi la bomu Uturuki

 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limelaani vikali mashambulizi ya bomu yalotekelezwa katika mji wa Reyhanli nchini Uturuki, mnamo siku ya Jumamosi, na ambayo yalisababisha vifo vya watu wapatao 46, na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Wanachama wa Baraza hilo la Usalama wameelezea huzuni yao kwa waathirika, na kutuma risala za rambirambi kwa jamaa za wahanga na serikali na watu wa Uturuki.

Wamesisitiza kuwa ugaidi wa aina yoyote ile ni mojawepo wa tishio kubwa zaidi kwa amani na usalama wa kimataifa , na kwamba vitendo vyovyote vya kigaidi ni uhalifu usiokubalika, bila kujali umechochewa na nini, unfanywa wapi, wakati gani na unatekelezwa na nani.

Huku wakiwataka walotekeleza mashambulizi hayo kuwajibika kisheria, wanachama hao wa Baraza la Usalama wameelezea ari yao kukabiliana na aina zote za ugaidi, sambamba na majukumu chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na kutolea wito nchi wanachama zizingatie sheria za kimataifa zinapopiga vita ugaidi, hususan sheria za haki za binadamu, wakimbizi na ile ya kibinadamu.