Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ya pembe inahatarisha uhai wa tembo

Biashara ya pembe inahatarisha uhai wa tembo

Kuna haja ya kuweka mbinu mpya za kukabiliana na uwindaji haramu wa haswa tembo ambao uhai wao u hatarini.

(Sauti Mlio wa tembo)

(Sauti ya Kaneiya)

Mlio wa tembo, tembo barani Afrika uhai wao uko mashakani kutokana na majangili wanaotaka kuwatoa uhai ili kuuza pembe zao kwa biashara mbali mbali.

Harakati za kulinda uhai wao zinachukuliwa kila uchwao. Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kwa kushirikiana na wadau limekuwa mstari wa mbele kufanya kampeni ili kuhakikisha tembo wa Afrika wanalindwa kwa maslahi ya kiuchumi ya nchi husika.

 (Mazugumzo)

Hivi karibuni balozi mwema wa UNEP, Li Bingbing ambaye ni mwigizaji mashuhuriChinaametembelea taasisi ya David Sheldrick karibu na mji mkuu waKenya,Nairobiambako tembo watoto walioachwa bila mama zao ambao wameuawa wamekuwa wakihifadhiwa na wakishakuwa wanarejeshwa porini.

(Mazugumzo)

Li Bingbing aliweza kujionea hali halisi na akaamua kupiga chepuo harakati za kulinda uhai wa tembo. Hapa katika mazungumzo mjini Nairobi akaeleza…

 (Li Bing-Sauti)

Li Bingbing akaenda mbali zaidi akasema raia wa Asia na wafanyabiashara wanaweza kusaidia sana Afrika katika kutokomeza biashara haramu ya pembe za ndovu kwa kususia bidhaa zitokanazo nazo.

 (Li Bing-Sauti)

UNEP inasema ongezeko la mauaji ya tembo kwa sasa limefikia kiwango cha juu na linatishia uhai wa tembo na maisha ya jamii zinazotegemea utalii hivyo basi hatua zichukuliwe haraka..

(Sauti Steiner)

(mlio wa Tembo)