Skip to main content

Sakata ya uundwaji wa katiba mpya inaendelea Tanzania

Sakata ya uundwaji wa katiba mpya inaendelea Tanzania

Suala la kuwa na katiba mpya si jipya hasa ukizingatia nchi nyingi duniani zinafanya mabadiliko na kujitahidi kwenda sambamba na hali halisi ikiwemo utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kama ya kutimiza haki za binadamu, kuwapa watu uhru wa kujieleza, kukuksanyika, kuupata elimu, maendeleo, huduma za afya na kadhalika.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukizichagiza nchi ambazo kwa mda mrefu hazifanyia marekebisho katika zake kufanya hivyo ili kukidhi matakwa ya wananchi wake na kuhakikisha maendeleo ya nchi yanakuwa ni jukumu la kila mwananchi.

Kuanzia bara Ulaya, Amerika, Asia na hata Afrika hali imekuwa sawiya. Kwa Afrika ya Mashariki walianza Kenya na baada ya mchakato wa muda uliojumuisha vikao, mivutano na hata kauli za jumuiya ya Kimataifa, hatimaye wakapata katiba mpya, sasa mbeleko wamewakabidhi jirani zao Tanzania ambao kwa sasa wako katika hatua za kuelekea uundwaji wa katiba mpya.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam George Njogopa amekuwa akifuatilia kwa makini mambo yanavyokwenda na kutuandalia makala hii.

(MAKALA NA GEORGE NJOGOPA)