Tanzania yasema haitishiki na vitisho vya M23

7 Mei 2013

Mwishoni mwa wiki, serikali ya Tanzania ilipata ridhaa ya Bunge la nchi hiyo ya kupeleka vikosi vyake kuungana na brigedi iliyoundwa kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuweka utulivu huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, DRC. Brigedi hiyo itajumuisha pia vikosi kutoka Afrika Kusini na Malawi ambapo imeripotiwa kuwa waasi wa M23 wamedai kuwa Tanzania isipeleke vikosi vyake na ikifanya hivyo itajutia. Ili kupata ufafanuzi wa madai hayo ya M23, Flora Nducha wa Radio ya Umoja wa Mataifa alizungumza na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Bernard Membe ambaye amezungumzia upelekaji wa vikosi hivyo na masharti kwa M23. Lakini kwanza alianza na hatua ya kuomba ridhaa ya bunge.

(Mahojiano Membe)