Baraza la Usalama lajadili majukumu mapya ya UM nchini Somalia

2 Mei 2013

 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo linajadili ubadilishaji wa majukumu ya ofisi yake ya kisiasa nchini Somalia UNPOS, ambapo ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inaeleza bayana umuhimu wa kubadilisha majukumu kutokana na mabadiliko ya kisiasa nchini Somalia.

 

Mashauriano ya leo yanafuatia azimio namba 2093 la Baraza la Usalama lililotaka Katibu Mkuu kufanya tathmini na kutoa mapendekezo ya majukumu mapya ya Umoja wa Mataifa. Nimemuuliza Balozi Augustine Mahiga, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu huko Somalia, UNPOS itakuwa nini na mantiki ya mabadiliko. 

(SAUTI MAHIGA) 

Balozi Mahiga akafanunua zaidi kuhusu tofauti ya nafasi ya serikali ya Somalia na ile ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA MAHIGA)

Mahojiano kamili na Balozi Mahiga yatapatikana katika ukurasa wetu.

Wakati huohuo Wasomali 258,000 wadaiwa kufa wakiwemo watoto 133,000 wa chini ya miaka mitano kutokana na hali mbaya ya usalama wa chakula na njaa. Hayo ni kwa mujibu wa utafiti wa shirika la chakula na kilimo FAO ulioangazia kipindi cha Oktoba 2010 na April 2012. Mark Smulders ni afisa wa masuala ya uchumi wa FAO.

(SAUTI YA MARK SMULDERS)