Chuo kikuu cha Al-Azhar na mtetezi kutoka Uganda wapewa tuzo:UNFPA

1 Mei 2013

Taasisi ya elimu iliyo na uhusiano na chuo kikuu cha Al-Azhar cha Misri na mtetezi wa maswala ya afya ya umma kutoka Uganda walitajwa kamawashindi wa tuzo ya UM ya idadi ya watu kwa mwaka 2013.

Tuzo hiyo inatunukiwa kila mwaka kwa watu binafsi na taasisi kwa kazi nzuri inahusiana na idadi ya watu na jitihada za kuimarisha afya ya umma.

Chuo hicho ambacho kimebeba sura ya imani ya dini ya kiislamu ambacho pia kinajihusisha moja kwa moja na elimu ya kidini, inatajwa kuwa ni moja ya vyuo vikuu ambavyo vinaheshimika na kusifika duniani katika ulimwengu wa kiislamu.

Kikiwa ni mafungamano mena na chuo kikuu cha Al-Azhar, chuo hicho kiliasisiwa mnamo mwaka 1975 kikiwa na dhima kuu ya kuendesha utafiti na kuibua mijadala yenye uhusiano na imani ya dini ya kiislamu.

Pamoja na weledi wa masuala mbalimbali lakini chuo hicho kinaheshimika na kuaminika hasa panapohusika na elimu inayohusika na taarifa na idadi ya waislamu duniani.

Kinaelezwa kwamba ni chuo ambacho kinauwezo mkubwa wa kutoa taarifa zinazohusu idadi ya waislamu na pia kinazingatia maadili na miiko ya sehemu husika.

Dr. Jotham Musinguzi ambaye anatajwa kuwa mstari wa mbele kuhusiana na elimu ya uzazi ikiiwa ndiyo moja ya nguzu muhimu ya kusuma mbele maendeleo ya kiuchumi, amekuwa amekuwa akishika nyadhifa mbalimbali na tangu kuanzia mwaka 2007 amekuwa akihusika moja kwa moja masuala ya afrika.