M23 waripotiwa kuweka kambi karibu na MONUSCO

1 Mei 2013

Huko Kivu Kaskazini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC  inaelezwa kuwa waasi wa kikundi cha M23 wamepiga kambi karibu na  ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu kwenye eneo hilo MONUSCO kama anavyoripoti Assumpta Massoi.

 (ASSUMPTA REPORT)

Radio Okapi imekariri vyanzo mbali mbali vikieleza kuwa waasi hao wa M23 kwa wiki kadhaa sasa wamepiga kambi eneo la Kiwanja, jimbo la Kivu Kaskazini, mita 30 kutoka ofisi za MONUSCO kwa lengo la kuzuia wafuasi wa kundi hilo ambao wanaripotiwa kutaka kujiengua na kujisalimisha MONUSCO.

Tangu mwanzoni mwa mwezi uliopita waasi 87 wa M23 wamejisalimisha MONUSCO huko Rutshuru na wameshajumuishwa katika mpango wa kupokonywa silaha na kujumuishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko  Goma.

Hata hivyo licha ya vitisho hivyo vya M23 ambao wanadiriki kuweka vizuizi vya barabarani kwenye barabara ya Rutshuru-Goma, waasi zaidi ya Kumi wameripotiwa kujisalimisha wiki iliyopita.