UNAMID kuhakikisha ulinzi na ustawi wa wakimbizi wa ndani:Chambas

1 Mei 2013

Mkuu wa Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur, UNAMID, Ibrahim Ibn Chambas amehitimisha ziara yake ya zaidi ya wiki moja katika majimbo matano ya eneo hilo ambapo amekuwa na mazungumzo na wananchi na viongozi kama anavyoripoti Grace Kaneiya.

 (Taarifa ya Grace)

Ziara hiyo ya kwanza kufanywa na Bwana Chambas tangu ashike wadhifa huo tarehe Mosi mwezi uliopita ilimpeleka katika majimbo yote ambapo pamoja na kueleza umuhimu wa kuwepo kwa amani ya kudumu alitoa shukrani kwa viongozi na wakimbizi wa ndani kwa ushiriki wao katika kupatia suluhu mgogoro wa eneo hilo.

Mathalani akiwa Shangil  Tobaya huko Darfur Kaskazini alijadili masuala ya ulinzi wa wakimbizi wa ndani na kusema suluhu pekee ni kupata amani ya kudumu ili wananchi waweze kuishi bila woga wala vitisho katika maeneoyao.

 Huko Darfur Mashariki alitoa shukrani kwa vile ambavyo uongozi ulitoa ushirikiano kuwezesha kufikisha misaada kwa wakazi wa Labado na Muhajeria waliokimbia makaziyaokufuatia mapigano ya hivi karibuni kati ya vikosi vyaSudanna kundi la Sudan Liberation. Bwana Chambas amesema UNAMID itaendelea kuhakikisha ulinzi na ustawi wa wakimbizi wa ndani hukoDarfur.