Baraza Kuu la UM lapitisha azimio kuhusu amani barani Afrika

26 Aprili 2013

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limerithia azimio la kisiasa kuhusu utatuaji wa mizozo barani Afrika kwa njia ya amani. Assumpta Massoi na taarifa kamili:(TAARIFA ASSUMPTA)

Azimio hilo linalohusiana na mkutano wa siku mbili wa Baraza Kuu kuhusu utatuaji wa mizozo kwa njia ya amani barani Afrika, linataja umuhimu wa kuongeza ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika.

Linataka pia kuwepo utaratibu wa kulinda amani na usalama barani Afrika, pamoja na kuthamini mchango wa mashirika ya kikanda.

Linataja umuhimu wa kutoa rasilimali na mafunzo ya kutosha kwa vikosi vya kulinda amani, kuimarisha uwezo wa kujikwamua na kujikarabati kwa nchi husika, kuendeleza suluhu za kisiasa na programu za maridhiano ya kitaifa, pamoja na kuunga mkono mikakati ya diplomasia ya kuzuia migogoro.

Akiongea baada ya kupitishwa kwa azimio hilo Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi amesema.

(SAUTI YA MANONGI)