Skip to main content

Hali mbaya ya usalama yasababisha ukosefu wa chakula Mali:WFP

Hali mbaya ya usalama yasababisha ukosefu wa chakula Mali:WFP

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP linasema hali ya ukosefu wa chakula inazidi kuwa tishio kaskazini mwa nchi hiyo kutokana na kuzorota kwa usalama.WFP inasema hali ni mbaya zaidi katika jimbo la Mopti ambako hata ustawi wa kijamii umezorotakamaanavyoripoti George Njogopa.

(PCKG YA GEORGE)

Ukosefu wa chakula ni tatizo linalosalia katika eneo la Kaskazini mwa Mali ambalo limesababishwa na hali ya kukosekana kwa amani ambayo pia ilivuruga shughuli za masoko.

Hali ni mbaya zaidi katika maeneo yaliyopo pembezoni ikiwemo jimbo la Mopti ambalo linakabiliwa pia na uanguko la ustawi wa kijamii.

Shirika la Kimataifa la mpango wa chakula WFP linasema kuwa linataanzisha jaribio la kusambaza misaada ya dharura katika eneo hilo wakati hali ya mambo inapoanza kuimarika.

Katika mwezi wa Marchi WFP ilifaulu kuyafikia maeneo kwa asilimia 54 katika maeneo jumla iliyopanga kuyafikia ikiwa ni hatua kubwa ikilinganishwa na mwezi mmoja nyuma yaani February ambako alifauli kwa asilimia 31 tu.

Shirika hilo linahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 79 ili kusambaza huduma za chakula hadi mwishoni mwa mwaka huu. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA BYRS)