Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukanda wa Zambezi wazindua juhudi za kuondoa Malaria

Ukanda wa Zambezi wazindua juhudi za kuondoa Malaria

Katika kuadhimisha siku ya Malaria duniani hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe na kusema kuwa bado ugonjwa huo ni mzigo kwa nchi maskini hususan barani Afrika ambako mamilioni ya watu wanashindwa kujikinga dhidi ya Malaria. Amesema barani Afrika kila dakika mtoto mmoja hufariki dunia kutokana na Malaria na kwamba mifumo dhaifu ya ufuatiliaji inakwamisha uwezo wa serikali na shirika la afya duniani, WHO kupata taarifa za kina kuhusu maeneo mapya yenye ugonjwa huo na mabadiliko ya mwenendo wa ugonjwa huo. Dkt. Thomas Teuscher kutoka mpango wa RollBack Malaria anasema pamoja na mafanikio yalopatikana, juhudi zaidi zahitajika,.

(SAUTI YA Thomas Teuscher)

Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi Afrika ni ukanda wa Zambezi ukijumuishaZimbabwenaZambiaambako mfuko wa kimataifa Global Fund umeamua kuuvalia njuga na leo kuzindua mpango maalumu wa kudhibiti malariakamainavyotanabaisha ripoti ya Joseph Msami

 (RIPOTI YA JOSEPH MSAMI) – Taarifa ya Malaria Msami

Mpango huo uliozinduliwa leo na Zambia na Zimbabwe una lengo la kuondoa malaria katika bonde la Zambezi na unaungwa mkono na Mfuko wa Kimataifa  wa kupambana na Ukimwi, kifua kikuu na malaria, Global Fund.Mpango huo utafadhiliwa kwa dola milioni 22 kwa Zambia na dola milioni 35 kwa Zimbabwe umetangazwa  na mawaziri husika wa nchi hizo mbili zilizoko katika bara la Afrika ambalo linatajwa kuathirika zaidi  kwa vifo vitokanavyo na malaria.

Kati  ya watu laki sita na sitini elfu wanaokufa kwa mwaka asilimia tisini ni kutoka barani humo.

Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo mawaziri husika wamesema utasaidia kupunguza maambukizi katika jamii za ukanda huo na utaanzisha mipango mipya kama ule unaohusisha chi za Msumbiji,ZambianaMalawinapia utasaidia katika kupunguza umaskini na kukuza uchumi katika bonde la Zambezi.