Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Ethiopia Yemen wakabiliwa na hali ngumu: IOM

Wahamiaji wa Ethiopia Yemen wakabiliwa na hali ngumu: IOM

Ujumbe wa mashirika ya kibinadamu, likiwemo Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, ukiongozwa na Mratibu wa shughuli za Umoja wa Mataifa nchiniYemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed, jana Aprili 18 ulizuru mpaka kati ya Yemen na Saudia na kujionea mateso wanayokumbana nayo maelfu ya wahamiaji kutoka Pembe ya Afrika.Ziara hiyo imefuatia uvamizi wa hivi karibuni wa mamlaka za  Yemen dhidi ya kambi za walanguzi na wasafirishaji haramu wa watu karibu na mji wa mpakani wa Haradh.

Zoezi hilo la uvamizi liliwanusuru wahamiaji 1, 987 kutoka kwa walanguzi ambao kawaida wakiwalazimisha wahamiaji kuwapa pesa, na kuwatesa wale ambao walishindwa kulipa.

Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)