Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Askari wa kulinda amani auawa Darfur

Askari wa kulinda amani auawa Darfur

Taarifa ya Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID imetangaza kuuawa kwa askari mmoja wa kulinda amani asubuhi ya leo huko Muhajeria, Darfur Mashariki, huku wengine wawili wakijeruhiwa.UNAMID inachunguza tukio hilo lililotokea baada ya watu wasiojulikana kushambulia kundi la ujumbe huo kwenye eneo hilo.

UNAMID inasema uchunguzi huo unafanyika kwa ushirikiano na serikali ya Sudan kuhakikisha watekelezaji wa kitendo hicho wanafikishwa mbele ya sheria kwa kuwa shambulio lolote dhidi ya walind amani wa kimataifa ni uhalifu kwa mujibu wa sheria za kimataifa.